Kuna vipengele vingi vibaya ambavyo vinahatarisha aina nyingi za wanyama na mimea kwenye sehemu mbalimbali barani Afrika. Hata hivyo hatujachelewa sana kuliokoa hilo jahazi na pia kuboresha maisha ya wakazi wa sehemu zenye wanyama pori.
Jambo hili laweza kutekelezwa kama wataalamu watatayarisha mikakati mbalimbali yenye uwezekano wa kusaidia zile sehemu ndogondogo au majimbo makubwa.
Baada ya miaka 15 yenye mafanikio katika shughuli za wanyama pori kama mtunzaji, daktari na mkurugenzi wa hifadhi ya taifa, nataka kuwapatia mataifa na mashirika binafsi, nikisaidiana na wataalamu wa timu yangu, maarifa, ujuzi na uzoefu wangu.
